KIKOSI cha  Simba kinatarajiwa kuondoka leo jijini Dar es Salaam kuelekea nchini Morocco kwa ajili ya kuweka kambi ya wiki mbili kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao. Yanga nao kupitia mitandao yao ya kijamii wamethibitisha kuweka kambi nchini humo bila kuweka wazi wataenda lini. Simba na Yanga zinaelekea Morocco ikiwa ni siku moja baada ya wachezaji wa timu hizo kupata chanjo ya corona katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.

kambi pic

Maandalizi ya timu hizo yanaanza mapema kutokana na mrundikano wa ratiba za michuano ya kimataifa inayotarajiwa kuanza Septemba 10, huku Ligi Kuu Tanzania Bara ikitarajiwa kuanza Septemba 29.

Baada ya michuano hiyo kuanza kwa hatua ya awali timu hizo zitakutana kwenye kombe la ngao ya hisani Septemba 25 ikiwa ni mfululizo wa mahasimu hao kukutana baada ya Julai 25 kukutana kwenye fainali ya kombe la shirikisho la Azam (ASFC) katika uwanja wa Lake Tanganyika Mkoani kigoma. Ikiwa unapenda michezo ya kubashiri, tembelea Meridianbet.

Awali Simba ilipanga kuweka kambi nchini Misri kabla ya kocha mkuu wa kikosi hicho Didier Gomes  kubadilisha maamuzi hayo kwa kile alichodai kuwa Morocco ni sehemu tulivu zaidi katika kipindi hichi cha corona tofauti na Misri. Aidha Yanga ulikuwa ni mp[ango wao wa muda mrefu kuweka kambi Morocco kutokana na mapendekezo ya Nasredine Nabi.